Mkuu wa Idara ya Utendaji ya Baraza la Taifa la Mpito (NTC) nchini Libya amesema kuwa, akiba ya mafuta ya nchi hiyo inaelekea kumalizika.Mahmoud Jibril amesema hayo pembeni mwa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi ulichofanyika magharibi mwa Amman mji mkuu wa Jordan na kuongeza kuwa, hadi hivi sasa asilimia 62 ya akiba ya mafuta ya Libya imeshachimbwa na ni asilimia 38 tu iliyobakia.Mkuu huyo wa Idara ya Utendaji ya NTC amesema pia kuwa, hatua za kwanza watakazochukua nchini Libya baada ya kupinduliwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi ni kurejesha amani na usalama nchini humo ili kupatikane mazingira mazuri ya kufufua uchumi na kuijenga upya nchi hiyo.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 273877
Mkuu wa Idara ya Utendaji ya Baraza la Taifa la Mpito (NTC) nchini Libya amesema kuwa, akiba ya mafuta ya nchi hiyo inaelekea kumalizika.